Dua za Kuanza Jambo

6 Dua

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Bismillahir Rahmanir Rahim

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Tukio:Kabla ya kufanya jambo lolote
Chanzo:Qurani

الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور

AlhamduliLLaahil-LLadhiy Ahyaanaa ba’da maa amaatana wa Ilayhin-nushuwr

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametupa uhai baada ya kutufisha na ni Kwake tu kufufuliwa.

Tukio:Kuamka Kutoka Usingizini
Chanzo:Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/113), Muslim (4/2083)

الحمدُ للهِ الّذي كَساني هذا (الثّوب) وَرَزَقَنيه مِنْ غَـيـْرِ حَولٍ مِنّي وَلا قـوّة

AlhamduliLLaahil lladhiyy kasaaniy haadha (ath-thawb) warazaqaniyhi min ghayri hawlin minniy walaa quwwah

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Amenivisha nguo hii, na kuniruzuku pasina uwezo kutoka kwangu wala nguvu

Tukio:Du’aa Ya Kuvaa Nguo
Chanzo:Irwaaa Al-ghaliyl (7/47)

بِسْمِ الله

BismiLLaah

Kwa jina la Allaah

Tukio:Kuvua Nguo
Chanzo:At-Tirmidhiy (2/505)

(بِسْمِ الله) اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِـكَ مِـنَ الْخُـبْثِ وَالْخَبائِث

(BismilLLaah) Allaahumma inniy a’uwdhu Bika minal khubthi wal khabaaith

(Kwa jina la Allaah) Ee Allaah najikinga kwako kutokana na mashaytwaan ya kiume na ya kike

Tukio:Kuingia Chooni
Chanzo:Al-Bukhaariy, (1/45), Muslim (1/283)

غُفْـرانَك

Ghufraanak

Nakuomba maghfira

Tukio:Kutoka Chooni
Chanzo:Taz takhriyj Zaad al-Ma’aad (2/386).